-30% Sale!

Kukimbia Pamoja na Mashujaa wa Imani

Hekima ya Biblia Katika Safari ya Maisha

Sh5,000.00 Sh3,500.00

Share

Description

Hekima ya Biblia Katika Safari ya Maisha

Mambo James ni Mwalimu wa neno la MUNGU, Mshauri na Mwandishi wa Vitabu, amekuwa
akifundisha na kushauri makundi mbalimbali ya watu hususani vijana ndani na nje ya Kanisa. Ana Shahada
ya kwanza katika Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa
sasa ni Mwanafunzi wa Shahada ya pili (Uzamili) Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Inasemwa kuwa maisha ni kama mbio ndefu (Marathon), lakini nafikiri maisha ni zaidi ya mbio ndefu, kwasababu unapokimbia mbio ndefu unajua mwisho wake kwamba ni takribani kilomita 40 hivi. Kwahiyo kama mkimbiaji unajua kabisa mwisho wa mbio kabla hujaanza kukimbia, lakini unapokuwa kwenye mbio za maisha hujui mstari wa mwisho utakuwa wapi mpaka utakapofika mwisho. Yaani hujui mwisho wa maisha yako utakuwa lini mpaka utakapofika mwisho.

Kitabu hiki kimejaa hekima za Biblia kutokana na mifano ya watu mbalimbali kwenye Biblia ambao tunawaita “Mashujaa wa Imani” Hadithi zao, maneo yao na busra zao zitakusaidia sana katika kukutia moyo na kukuimarisha unapoendelea na safari hii ya wokovu na maisha kwa ujumla.

Mwandishi ametumia lugha nyepesi ya masimulizi na mazungumzo iliyojaa ubunifu na weledi mkubwa ili kuzipa uhai zaidi hadithi mbalimbali na kukupa picha halisi unaposoma. Utakapoanza kukisoma kitabu hiki hutatamani kukiweka chini kwani hutakuwa tu msomaji bali utajikuta umekuwa muhusika pamoja na wahusika ndani
ya kitabu; Nakuatakia usomaji mwema utakaobadili maisha yako ya kiroho na kimwili.

Kimechapwa na: Mambo James
Utangulizi: Bishop Boniface William Zakariah

Additional information

Hard Copy

Hard Copy

Soft Copy

Soft Copy